Kwa
sasa nimeokoka na kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa
maisha yangu lakini kabla sijaokoka nilikuwa mtumwa wa shetani
kupitia uchawi.
Nimeamua kuandika waraka wangu huu baada ya kuguswa .
Ninaona
nina wajibu mkubwa wa kuelezea siri hizi za wachawi ili
niweze kuwekwa huru lakini pia niweze kuwasaidia watu wengine
waweze kuwa huru, kwani maandiko matakatifu yanasema nanyi mtaijua
kweli nayo itawaweka huru.
Nimeona
si vyema endapo nitakufa nikiwa na siri yangu hii. Mambo
niliyo yapitia yamefunza mambo mengi sana maovu yanayo tendeka
katika ulimwengu huu ambayo nilikuwa siyafahamu hapo awali.
Ninataka ulimwengu mzima uyafahamu na hivyo kuwa huru.
Nisiwachoshe
kwa maneno mengi ila kwa ufupi tu ni hivi mwaka 2014 rafiki yangu
mmoja alinipeleka kwa mganga wa kienyeji ili anisaidie niweze
kupata mume wa kuniona.
Nilifikia
uamuzi huu baada ya mwanaume alie kuwa anataka kunioa kufariki
ghafla kwa ajali ya gari huku akiniacha na kichanga cha minane
tumboni.
Tukio
hilo lilini huzunisha sana kwa sababu mwaka huo wa 2014 nilikuwa
nimetimiza umri wa miaka 40 nikiwa bado naishi nyumbani kwa
wazazi wangu huku nikiwa na watoto wawili huku kila mmoja
akiwa na baba ake.
Nilimfuata dada mmoja jirani yangu ambae alikuwaga ananisaidia hela na chakula kila nilipokuwa naenda kumuomba
Nilipo
mfuata kuomba ushauri nifanye nini, nilimuelezea historia yangu
yote kuanzia mume alietaka kuniona wakati bado nipo msichana
kisha akaingia mitini kabla ndoa haijafungwa, mwanaume nilie zaa
nae mtoto wa kwanza, wapili hadi huyu ambae amefariki na
kuniacha na kichanga cha miezi minane.
Dada
huyu akaniambia atasaidia kunihudumia hadi nitakapo nijifungua
na nikisha jifungua atanipeleka kwa mganga ambae atanisaidia.
Kweli alifanya kama alivyo niahidi. Bahati mbaya mtoto hakuwa riziki. Alizaliwa akiwa amefariki tayari.
NAPELEKWA KWA MGANGA
Tulipofika kwa mganga akanitazama na kuniambia kuwa nimefungwa kichawi.
Mganga akaniambia kuwa nyota yangu iliibwa kichawi muda mrefu kwa ajili ya kwenda kutumikishwa kichawi.
Mganga
akaniambia hakuna haja yoyote ile ya kuirudisha nyota hiyo kwa
sababu imeshakufa huko ilipo na haiwezi kunisaidia kitu chochote
hata kama itarudishwa kwa sababu imetumikishwa .
Akaniambia
ilikuwa niolewe tangu nikiwa na miaka 20,lakini “ndoa” yangu
ilibatilishwa kichawi kwa kutumia bundi na bahati yangu ya
kuolewa akapewa mwanamke mwingine.
Na
kweli kwa mujibu wa kumbukumbu zangu, nikiwa nina umri huo kuna
mwanaume mmoja alitaka kunioa lakini badae ndoa ikapeperuka hata
sijui kitu gani kilitokea.
Mganga
akaniambia kwa kuwa bahati yangu ya ndoa iliibwa kwa kutumia
bundi basi na mimi itabidi niibe bahati ya mtu mwingine kwa
kutumia bundi.
Sikuwa na jinsi Zaidi ya kukubaliana na mganga pamoja na kwamba sikujua lingewezekanaje hilo..
NAAMBIWA NIKACHUME MTI WA PILIPILI NIKIWA KWENYE SIKU ZANGU.
Mganga
akaniambia nirudi nyumbani, halafu siku nitakapo ziona siku
zangu basi niende kwenye mti wa pilipili nichume pilipili
halafu niutazame vizuri huo mti kisha nimjulishe nimeona nini.
NACHUMA MTI WA PILIPILI NIKIWA KWENYE SIKU ZANGU
Siku
nilipoziona siku zangu nikaenda kuchuma pilipili. Niliona kitu
cha ajabu sana. Kitu ambacho sikuwahi kukiona tangu nizaliwe.Ule
mti wa pilipili ulikauka ghafla. Niliogopa sana nikampigia mganga.
Mganga akaniambia niuchume huo mti halafu kesho niende nikamuone.
NAPELEKA KWA MGANGA MTI WA PILIPILI ULIO KAUSHWA NA HEDHI
Kesho
yake nikadamkia kwa mganga na mti wa pilipili ulio kauka.
Mganga akauchukua huo mti na kuusaga pamoja na dawa zake
nyingine anazo zijua yeye mwenyewe. Baadae akanichanja akanipaka
mafuta ambayo sikujua ni mafuta ya nini. Akanipa dawa za kuoga,
na kunywa pamoja na hirizi.
Halafu akanipa dawa ya kuchoma usiku.
MGANGA ANANIELEKEZA NAMNA YA KUWAITA BUNDI NA KUWASILIANA NA BUNDI KWA ISHARA.
Mganga akaniambia haya mafusho ninayo kupa ni uchawi mkubwa sana.
Zingatia masharti yote nitakayo kupa vinginevyo utapata madhara makubwa sana.
Akaniambia
hilo ni fusho maalumu la kuwaita bundi. Kwa kutumia fusho hilo
utakuwa unawaita bundi na kwa kuwatumia bundi hao utaweza kujua ni
katika nyumba gani kuna mwanamke mwenye bahati ya kuolewa.
Kupitia bundi utaweza kujifunza vitu vingi sana ambavyo ulikuwa hauvijui.
Mbali
na kujua mwanamke gani ana bahati ya kuolewa, unaweza kujua
kwenye nyumba gani kuna watu wana nyota nzuri nakadhalika.
Mganga akaniambia nitakufundisha namna ya kutafsiri ishara mbalimbali za milio ya bundi.
i.
Bundi akilia mara moja, anatoa ishara kuwa katika nyumba hiyo
kutatokea msiba hivi karibuni. Na hapo itategemea amelia saa
ngapi. Kama akilia kati ya saa sita na saa saba usiku basi
anakuwa anatoa ishara ya kutokea kwa msiba na kama kama atalia
kati ya saa 4 na saa 5 usiku anakuwa anatoa ishara na
kuwaonya wenye mji juu ya ujio wa wachawi katika mji huo
usiku huo.
Hii
ni kwa sababu bundi anaweza kuona mambo ya sirini, mambo aliyo
fichwa mwanadamu na mambo yatakayo tokea siku za mbeleni.
ii.
Bundi akilia mara mbili maana yake ni kwamba wewe ulie isikia
sauti hii utapata mafanikio makubwa sana katika kitu unacho taka
kukianzisha hivi karibuni, na ili ufanikiwe katika kitu au jambo
hilo ni lazima ukifanye haraka iwezekanavyo.
iii.
Bundi akilia mara tatu basi anatoa ishara kwamba katika nyumba
iliyopo karibu na mti ambao bundi huyo alitua wakati analia,
kuna mwanamke ataolewa na ndoa yake itadumu kwa muda mrefu.
iv.
Bundi akilia mara nne anakuwa anatoa ishara kwamba wakaazi wa
nyumba au mtaa huo watapata usumbufu mkubwa katika siku za
karibuni.
v. Bundi akilia mara tano anatoa ishara kwamba wewe ulie sikia sauti hiyo utapata safari nzuri hivi karibuni.
vi. Bundi akilia mara sita anatoa ishara kwamba, kuna wageni wapo njiani wanakuja kuwatembelea.
vii.
Bundi akilia mara saba anatoa ishara kwamba kuna mtu au watu
katika nyumba hiyo watapatwa na matatizo ya msongo wa mawazo.
viii. Bundi akilia mara nane, anakuwa anatoa ishara kwamba katika nyumba hiyo utatokea msiba wa ghafla.
ix. Bundi akilia mara tisa anatoa ishara ya bahati njema katika nyumba hiyo.
Sasa basi, wachawi huwa wanakuwa makini sana kusikia sauti za bundi pindi wanapolia. .
Baada
ya hapo mganga akaniambia natakiwa kwenda kumwaga mafusho
hayo kidogo kwenye mti wowote mkubwa ulio jirani na nyumba
ambayo nimeikusudia na kuchukua jani la huo mti kwenda nalo hadi
chumbani kwangu kisha kulichoma kwenye chetezo pamoja na hayo
mafusho huku nikitamka maneno maalumu ya kuwaita bundi waje
kwenye huo mti ili waweze kujua ni mwanamke gani anakaribia
kuolewa ndani ya nyumba hiyo.
Usiku
wa siku hiyo nikafanya kama nilivyo elekezwa. Nikaenda kuchuma
jani la huo mti na kuwamga fusho kidogo kwenye mti kisha
ilipofika saa tatu za usiku nikaanza kuchoma ilo fusho pamoja
na jani la huo mti.
Ilipofika saa sita usiku kweli bundi wakaja na muda si mrefu wakaanza kulia. Nikasikia kwa makini sana.
Bundi
akalia mara tatu . Alilia kutoka kwenye mti uleule ulio jirani
na nyumba ya shangazi yangu. Nilichagua mti ulio jirani na nyumba
ya shangazi yangu kwa sababu shangazi yangu alikuwa na watoto
wengi wa kike na nyumba yake ilikuwa na wageni na wapangaji
wengi wanawake.
Mganga aliniambia bundi wakisha nyamaza tu nimjulishe haraka sana.
Kama alivyo nielekeza mganga nikamjulisha.
Nilipo
mjulisha akaniambia sawa, nilale halafu kesho asubuhi nihakikishe
naenda kwa shangazi yangu au naongea na mtu yoyote anaeishi
nyumbani kwa shangazi yangu.
Nitakapo
kuwa hapo kwa shangazi yangu nisikie kama watazungumza chochote
kuhusu bundi na kama wasipo zungumza basi nijifanye kuanzisha
mazungumzo kuhusu bundi, nijifanye na mimi jana bundi walitua
nyumbani kwetu na kwamba ninaogopa sana.
Na watakacho nijibu basi nimjulishe mganga.
Kweli
nikaenda hadi kwa shangazi na bahati nzuri nikamkuta binamu
yangu ambae ndio nilibatilisha ndoa yake kichawi.
Binamu
hakuwa na dalili zozote za kupiga story kuhusu bundi hivyo
nikaanzisha story za bundi kwamba jana bundi walilia sana
batini kwangu na kwamba nilishindwa kulala.
Binamu
akaniambia hata kwao ilikuwa hivyo hivyo na sio kulia tu
bali kuna wakati bundi waliingia hadi ndani wakatua na
kuondoka.
Tukaongea kwa muda kidogo kisha baada ya hapo nikampigia mganga na kumueleza kila kitu.
Mganga akaniambia vizuri sana, mambo yako yatakuwa mazuri sana.
Niseme
kitu kimoja, wachawi kwa kumtumia bundi, wakishajua kwenye
nyumba Fulani kuna mtu ana nyota ya kuolewa hivi karibuni au
kuna watu wenye nyota kali wamelala kwenye nyumba hiyo huwa
wanawatuma bundi kwenda kuiba nyota hizo.
Hivyo
basi siku ukisikia bundi wamelia mara tatu karibu na nyumba
yenu halafu baadae wakaingia ndani basi jua bahati ya kuolewa
ya mtu imeibiwa na kama kuna watu wenye nyota kali walikuwa
ndani ya nyumba hiyo basi na nyota zao zinakuwa zimechukuliwa
pia.
Hivyo
ndivyo alivyo niambia Dokta na akaniambia ikitokea nimeenda
kwenye mji wa ugenini halafu jambo hilo likatokea, basi
nihakikishe huyo bundi atakae ingia ndani anauliwa au anakamatwa
kabla hajapaa,jambo ambalo hata hivyo ni gumu sana kwa
sababu bundi wanapo ingia ndani huwezi kuwasikia kwani huwa
wanapaa bila kupiga kelele wala kutoa sauti.
Dokta akaniambia huu ni uchawi unao tumika sana na hautumiki kwenye masuala ya mapenzi tu bali biashara pia.
Akaniambia
wafanya biashara wengi wametajirika na wanaendelea kutajirika
kwa kutumia uchawi huu wa kuiba nyota za watu kwa kuwatumia
bundi.
Na hii ndio sababu bundi anatukuzwa sana miongoni mwa wafanya biashara.
Mganga
akaniambia ili nyota isichukuliwe na bundi kwa staili hiyo
natakiwa niwe na kinga maalumu ya kuwazuia bundi kuchukua
nyota.
Akasema
kinga hii ni tofauti na kinga zingine zote na kwamba hata
kama una kinga nyingine yoyote ile lazima kinga hii uwe nayo
pia.
Akaniambia kwa kuwa nimeingia kwenye mtandao huu inabidi hiyo kinga niwe nayo.
Siku
ya kutengeneza kinga hii,mganga alichukua paka mweusi, akauliwa
kisha akatobolewa macho halafu kwenye macho yake zikawekwa mbegu
za mti wa mnyonyo kila jicho.
Paka
huyo akafungwa kwenye kitambaa cheupe mfano wa maiti akawekwa
kwenye mfuko nikapewa kwenda nae na kumzika vichakani kwenye
eneo ambalo nitaliweka alama… Nikawa namwagilizia maji kila siku
hadi mti ulipo chipuka na kukua.. Mti ulipo kua mganga
akaniambia nitoe mbegu, nikafanya kama alivyo nielekeza . Mganga
akaniambia nichukue mbegu saba kisha nimpelekee.
Nilipo
mpelekea mbegu hizo mganga, akazichukua akachanganya na dawa zake
anazo zijua mwenyewe akachukua popo,akamkata kucha akiwa hai na
kumuacha, akaziasaga na muzichoma kisha kunichanja na kunipaka.
BAADA YA BUNDI KULIA NA KUTUA KWENYE NYUMBA YA SHANGAZI YANGU
Sikuwa
najua kama binamu yangu mtoto wa shangazi yangu alikuwa na
mpango wa kuolewa kwa sababu ni jambo lililofanywa siri.
Lakini
siku chache baada ya bundi kutua kwenye nyumba ya shangazi
yangu nikaanza kusikia habari za kuharibika kwa mipango ya ndoa
ya binamu yangu.
Binamu
yangu alitaka kujaribu kujiua baada ya mume mtarajiwa kugombana
nae na kuingia mitini na kisha kuhamishia uchumba kwa mwanamke
mwingine.
Wakati huo huo,mimi nikapata mwanaume mwenye pesa ambae alinichumbia na kunioa tena kwa harusi kubwa.
Ni
hivi bahati ya ndoa ya mtu inayo ibwa kwa kutumia bundi, sio
lazima wewe uolewe na aliekuwa anataka kumuoa mwanamke uliye iba
bahati yake.HAPANA. Ni hivi inaweza kutokea mwanaume huyo labda
akafukuzwa kazi ghafla au akafilisika na mipango yake kuvurugika.
Nyota ya mwanaume huyo inaibwa anapewa mwanaume mwingine ambae atakuja kukuoa wewe.
NAAMUA KUACHANA NA USHIRIKINA NA KUMRUDIA MUNGU.
Niliishi
na mwanaume huyo toka 2014 hadi 2016 katikati.. Siku moja
nilipokea taarifa za msiba wa rafiki yangu ambae ndio
aliniunganisha na huyo mganga.
Huyu dada alikuwa anaishi maisha ya kidini lakini kumbe alikuwa anafanya ushirikina sana.
Kuhusu
kifo chake, sijui kama kilitokana na ushirikina ama ni mipango
ya mungu lakini nilipo ona mwili wake niliogopa sana.
Niliwaza
nakuwazua, nilitafakari nakutafakari. Nikajiuliza moyoni kumbe na
mimi pamoja na mali na pesa hizi nilizo zipata kwa njia ya
ushirikina ipo siku nitakuwa kama huyu ?
Kumbe mimi sio kitu kabisa katika dunia hii ? Kumbe binadamu ni mchanga.
Kumbe binadamu ananuka na kutoa harufu ? Kumbe ipo siku ndugu zangu wataogopa kulala na mimi ?
Nilitakafakari sana .. Nilikumbuka mambo mengi ya utotoni. Jinsi nilivyo lelewa na wazazi wangu.
Nililelewa kufuata maadili ya Mungu na kuwa mvumilivu na mstahimilivu kwa namna yoyote ile.
MAHUBIRI YA MCHUNGAJI WAKATI WA MAZISHI YANILIZA
Nikiwa katika hali ya majuto na uchungu mkubwa Mchungaji alianza kuhubiri neno la Mungu.
Alihubiri
mambo mengi sana lakini kikubwa aliwasisitizia waombolezaji
kumkumbuka Mungu wakati wa uhai wao na kwamba hapa duniani
tunapita tu.
Mchungaji waliwaasa waumini wasiwe na tamaa na mali za duniani hapa kwani tutaziacha hapahapa duniani.
Mchungaji
akawakumbusha waumini kwa kuwasomea neno la Mungu kutoka katika
kitabu cha MATHAYO 16 : 26 ambalo linasema
“Kwa maana mtu atapata faida gani akiupata ulimwengu wote lakini aipoteze nafsi yake?au mtu atatoa nini ili aipate nafsi yake?”
Hapa Mchungaji akawa kama ananiongelea mimi kabisa.
Baadae
akasema najua kuna watu wanakata tamaa ya kufanikiwa katika
maisha kwa sababu wamehangaika muda mrefu bila mafanikio.
Shetani anazitumikisha nafsi zao kwa faida yake na watu wake. Wametupiwa nuksi na mikosi na wachawi.
Mungu
anasema katika kitabu cha YOELI 2 Sura ya 25 Nami nitawarudishia
hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi
langu kubwa nililotuma kati yenu…
Baadae
Mchungaji akasema kama kuna watu wapo tayari kuokoka basi na
wanyooshe mikono yao nami nitawaongoza sara ya toba.
Nilidhani
ni mimi tu nitakae nyoosha mkono wangu lakini nilishangaa
kuona na watu wengine wengi tu wakinyoosha mikono yao.
Hata
yule binamu yangu ambae niliiba nyota yake kichawi nae
alinyoosha mkono wake. Wote tuliombewa na baadae tukaanza
mafundisho kanisani na hadi muda huu ninaondika waraka huu
bado tunaendelea kumtumikia Mungu.
KUHUSU
MUME WANGU : Mume wangu alinikimbia baada ya kuona nimeokoka
jambo ambalo nililishukuru pia kwa sababu hakuwa haki wala staili
yangu.
MAISHA YETU YA MAHUSIANO KWA SASA.
Kwa sasa mimi nina mchumba na yule binamu yangu ameshaolewa tayari.
KUHUSU MGANGA ALIYE NIINGIZA KWENYE SUALA LA KUIBA NYOTA ZA WATU KWA KUMTUMIA BUNDI.
Mganga huyu anajulikana Zaidi kama mungu wa kabili na namba zake za simu ni 0744 -000 473.
NIMEWEKA
JINA LAKE NA NAMBA ZAKE ZA SIMU ILI WATU WAJUE KWAMBA HUYU
NI MCHAWI NA WAKALA WA WACHAWI NASHETANI NA WAEPUKANE NAE KWA
SABABU ATAWAINGIZA KWENYE MAMBO YA UTUMWA WA ULOZI NA UCHAWI
KAMA ALIVYO FANYA KWANGU.
No comments:
Post a Comment