Simba sc ilimsajili Okrah kutoka Benchem United inayoshiriki ligi kuu nchini Ghana ambapo staa huyo alikua na takwimu bora kabisa zilizowavutia Simba sc akifunga mabao 14 katika mechi 32 za ligi kuu nchini humo.
Taarifa za kuachwa kwa Okrah zimetangazwa katika vyanzo rasmi vya klabu vya mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na kumaliza tetesi za muda mrefu za kutemwa kwa staa huyo ambaye wapenzi wengi wa klabu hiyo walikua na matarajio makubwa na staa hiyo
“Baada ya kuwa kwenye kikosi chetu kwa msimu mmoja, Augustine Okrah hatakuwa sehemu ya timu yetu ya msimu ujao”ilisomeka taarifa kutoka katika mtandao wa kijamii wa facebook wa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment