Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-08-14

Mauno stageni yamponza Snura


   
Msanii wa muziki, Snura Mushi ameeleza jinsi anavyosumbuliwa na wanaume kutokana na uchezaji wake akiwa stejini.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Shindu’, amesema licha ya kupata usumbufu huo kwa wanaume hao lakini amekuwa akijitunza na kujiheshimu kwani anafanya hivyo kulinda kazi yake na heshima yake kama mwanamke.
“Unajua watu wakisikia Snura Chura huwa wanatokea wengi sana, na kweli huwa napata shida sana kwa wanaume wengi wenye matamanio,” Snura alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA. “Na inawezekana kweli kati yao wapo wenye mapenzi ya kweli na mimi lakini ndiyo hivyo,”
Aliongeza, “Kitu nachozingatia sana ni kuilinda kazi yangu, hivyo wanapotokea wanaume wa namna hii mimi nachokifanya siku zote ni kuwa mbali nao kabisa ndiyo maana nashinda vishawishi hivyo kila siku” alisema Snura

Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wa kike ambao wanatumia viuno kuwapagawisha mashabiki wake akiwa stejini.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina