Hali ya utulivu imerejea mjini Juba, Sudan Kusini baada ya Rais Salva Kiir na Makamu wa Rais Riek Machar kuagiza wanajeshi watiifu kwao kusitisha vita.
Mji wa Juba umetikiswa na mapigano makali tangu siku ya Ijumaa ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 300.
Ingawa vita vimesitishwa, maafisa wa utoaji misaada wanasema hali bado ni mbaya mjini humo na watu wengi hawana vyakula na maji.
Maelfu ya raia walikimbilia makanisani na katika vituo vya Umoja wa Mataifa kutafuta hifadhi
Rais Kiir na Dkt Machar kwa sasa wanakabiliwa na shinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa, Marekani nan chi jirani kuheshimu mkataba wa Amani ambao walitia saini mwaka jana.
Mkataba huo ulikomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa vimezuka Desemba 2013.
Viongozi hao wametakiwa kuhakikisha taifa hilo halitumbukii tena kwenye mapigano.
No comments:
Post a Comment