Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima,
jana alizushiwa kuwa amefariki dunia.
Taarifa hizo zilizozagaa katika mitandao ya kijamii zilieleza kuwa
Askofu Gwajima alifariki dunia katika hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo zilienea kuanzia ya saa tano
asubuhi, zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia kwa shinikizo la
damu.
Hata hiyo, taarifa hizo zilikanushwa vikali na mwanasheria
wake, wakili wa kujitegemea Peter Kibatala.
Kibatala jana alisema taarifa hizo ni za uzushi ambao haelewi
chanzo chake.
“Nimesikitishwa na taarifa hizi na nimepigiwa
simu nyingi sana leo kuniuliza juu ya kifo cha Askofu Gwajima na nimebaki
nashangaa kwani ni mzima wa afya,” alisema Kibata.
Majira ya jioni jana picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii
ziliomwonyesha Askofu Gwajima akiwa mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
No comments:
Post a Comment