Na Fred
Jakuba
Taasisi
ya kuzuia na kupamba na rushwa(Takukuru) imewafikisha mahakamani mhandisi wa
halamshauri ya wilaya ya Geita na mkandarasi kwa makosa ya rushwa.
Akisoma
makosa hayo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ,Mh.Ushindi Swalo
mwendesha mashitaka wa takukuru Bw.Kelvin Marusuri ameieleza mahakama kuwa
mnamo june 7/ 2009 na September 21/2009 wakiwa ofisi za halmashauri
ya wilaya walitumia nyaraka kumdanganya mwajiri na kumsababishia hasara.
Watuhumiwa
waliandaa nyaraka yenye maelezo ya uongo kuwa kazi imefanyika kwa kuzingatia
makubaliano na hivyo mkandarasi anastahili kulipwa pesa zote za mkataba
licha ya kutambua kuwa kuna baadhi ya kazi za thamani ya tsh 10,326,200(milioni
kumi laki tatu ishirini na sita elfu mia mbili) hazikufanyika kulingana na
mkataba.
Waliofikishwa
mahakamani ni mhandisi,Mathias Shoto akituhumiwa kwa kosa la kumdanganya
mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa
namba 11 ya mwaka 2007 na kumsababishia mwajili hasara kinyume na kifungu cha
284a(1)cha kanuni ya adhabu sura 16 marejeo ya mwaka 2002.
Wengine
ni Hamisi Allani Chande na mkandarasi ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi
ya Kidagaa,Bw.Peter Alexander.
Aidha
mwandisi Mathias Shoto ameachiwahuru kwa dhamana hadi kesi hiyo
itakapotajwa tena ifikapo march 10/2016 huku watuhumiwa Hamis Chande na Peter
Alexanda wakishindwa kukamilisha masharti ya dhamana na kwamba Mahakama imeamuru
warudishwe mahabusu
No comments:
Post a Comment