Wananchi mkoani Geita wamempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa uteuzi wa wakuu wa mikoa ambao alitangaza siku ya jana marchi 13.
Wakizungumza na storm habari baadhi ya wakazi wa mkoani hapa wamesema kuwa uteuzi wa Raisi umeangalia swala la uadilifu na kutazama wale ambao anaamini watakwenda na kasi yake ya kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kuweza kuleta maendeleo katika maeneo ambayo wamepangiwa kufanyia kazi.
Aidha wamemwomba mkuu mpya wa mkoani hapa Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Elias Kyunga kuhakikisha kuwa anatatua changamoto za ajira kwa vijana na kuwa anatenda kazi kwa kufuata usawa na haki kwa wananchi waliopo mkoani hapa.
Wakuu wa mikoa wapya ambao wameteuliwa na Rais wanatarajia kuapishwa kesho marchi 15 kuanzia majira ya saa 3:30 asubuhi ikulu jijini Dar es salaam.
safi sana
ReplyDelete