Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-03-17

WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI MAAFISA 3 WA SERIKALI WILAYANI CHATO MKOANI GEITA.

Waziri mkuu mh Kassim Majaliwa

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Kassimu Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watatu wa Serikali wilayani Chato kwa makosa tofauti ikiwemo ya ubadhilifu wa fedha ,na madai ya fedha kwa sakosi mbili ambazo alikuwa akidaiwa Afisa ushirika ikiwa ni pamoja na kuuwa ushirika wa sakosi ya umoja.

Waliosimamishwa ni mhandisi wa maji Peter Ngolemo kwa tuhuma za kupotea kwa pampu katika kijiji cha Karebezo Kata ya Mirembe, Warioba Mwita ambae ni Afisa Ishirika kwa kile kinachodaiwa kuwa alikopa fedha katika sakosi na kushindwa kurejesha fedha hali iliyopelekea kuwepo kwa migogoro katika sakosi mbili ya walimu na umoja,na Afisa maendeleo ya jamii pamoja na Dionizi Mulayoba kosa lake ni ubatilifu wa fedha.
Aidha waziri Majaliwa amewataka watumishi wa serikali kubadilika na kuhakikisha wanafuata misingi ya uadilifu pindi wawapo kazini ikiwa ni pamoja na kuwa wawajibikaji katika maeneo ambayo wanatakiwa kujituma kwa bidii zaidi ili kuleta maendeleo kwa nchi na kwamba hakuna mtu yeyote atakaye lindwa endapo akienda kinyume na kanuni na sheria ya nchi katika swala la uwajibikaji.
Waziri mkuu leo anatarajia kumaliza ziara yake ya kikazi mkoani hapa kwa kukutana na viongozi wa ngazi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi wa Katoro wilayani Geita. 

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina