
Jina lake la kuzaliwa ni William Malecela na jina lake maarufu
la mitandaoni ni Le Mutuz ambaye ni mmiliki wa
williammalecela.com na jana April 11 2016 aliamua kuwajibu
wanaomuandama kutokana na uteuzi wa ukuu wa mkoa wa Shinyanga chini ya Anne
Kilango Malecela ambaye ni mama yake kutenguliwa.
Le Mutuz Aliandika: "Guys naomba kusema hivi nimepigania Rais Magufuli
kuwa Rais na ninamuunga mkono kwa juhudi zake za kusafisha uozo hata kama
unamuhusu Mama yangu mzazi kwa sababu hata mimi wafanyakazi wa Kampuni yangu
wasipofuata masharti yangu kama muajiri ni lazima niwaondoe sasa Nina
wafanyakazi 4 ambao ili kuwa nao nilipitia kama watu 100
"Now nimesikia kwamba Mama yangu hakufuata masharti ya
muajiri wake so amefukuzwa kazi kwangu sina pingamizi wala ishu na Rais kwa
sababu Sheria ni msumeno inatakiwa kukata kote….now naona maneno mengi sana
ambayo hayana UKWELI wala Msingi ndani yake
"Nimekaa Majuu Miaka 30 nimerudi Bongo nimesota nimeanzisha
Kampuni yangu ya BLOGU YA WANANCHI MEDIA COMPANY LTD na sasa hivi nipo njiani
kuhamia kwenye RADIO na TV now katika Maisha yangu sijawahi kuishi kwa
kumtegemea mtu ila ninaishi kwa kumtegemea MUNGU‘
"Nilikuwa nafagia Majuu na pia nahangaika Baharini wakati
Baba yangu Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Leo eti Maisha yangu yataharibika kwa
sababu Mama yangu sio RC? hahahaha imenichekesha sana hizi CHUKI guys zitawaua
bure mnazitoa wapi? ….I mean Jana nimerudi Nairobi na sasa najitayarisha kwenda
South Africa weekend hii na nikirudi ni safari ya Dubai eti Mama yangu kuwa RC
wa Wiki Mbili Shinyanga kunahusika na Maisha yangu hapa Mjini Downtown na hizi
Safari zangu za kikazi?
"Hahahahahaha imenichekesha sana guys nimeshasema Mara
nyingi kwamba ninajua sana kwamba uhusiano wa Public na Watu Maarufu huwa ni
feki ila sikutegemea kwamba watu wanaweza kuwa na CHUKI za mpaka kulazimisha kwamba
eti u RC wa Mama yangu kwa Wiki Mbili tu unahusika na Maisha yangu hapa
Downtown kwamba Nina Ofisi
"Apartment na Kampuni kwa sababu Mama yangu alikuwa RC wa
Shinyanga kwa Wiki Mbili tu na sasa Maisha yangu yataisha HAHAHAHAHAH jamani
this is the best joke of my life….otherwise guys nimewasikieni ila ninasimama
na Rais Magufuli na I feel sorry for my Mum ila ni Kawaida in life na Sheria ni
msumeno ….otherwise Lov U guys HAHAHAHAHa and I am Super Humbled U know" – le
Mutuz Nation
No comments:
Post a Comment