Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha TLP na aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo, Agustino Mrema anatarajia kusafiri kuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kumpongeza Rais Magufuli na kumkumbusha ahadi aliyompa mwaka jana ya kumpatia kazi Serikalini.
Akizungumza kupitia kipindi cha Sun Rise kinachoruka kupitia Times fm, Mrema amempongeza Rais kwa jitihada za ukusanyaji kodi na kupambana na Ufisadi kwa nguvu.
“Tuweke itikadi pembeni Rais wa sasa anaweka juhudi katika kukusanya kodi, na mimi nilikuwa napiga nalo sana kelele hili swala, ila akipewa ushirikiano baada ya miaka mitano tutasheherekea mafanikio yake.
“Wiki ijayo natarajia kuja Dar, na nafikiri nitaonana na Rais kwanza nimpongeze alafu nimsisitize anipe nafasi kuna sehemu nazijua tuzisafishe, siwezi kusema mpaka nionane nae ndio nitamueleza”.
Mrema pia alijivunia rekodi yake ya uongozi katika Serikali ya Tanzania, kama kigezo kimoja wapo cha kumpatia ‘Chambirecho’ ya kupewa nafasi katika Serikali ya Magufuli.
No comments:
Post a Comment