Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akipokea maua kutoka kwa mtoto Sharon Innocencia Shiyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kwenye mkataba wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana makabrasha ya mkataba na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji Saini wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit kabla ya utiaji saini wa Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akitoa hotuba yake mara baada ya zoezi la utiaji Saini kukamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit wakipiga makofi mara baada ya kufurahishwa na wimbo wa bendi ya Polisi iliyokuwa ikitumbuiza Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan watatu kutoka kushoto na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watatu kutoka kulia.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wakati Bendi ya Matarumbeita ilipokuwa ikitumbuza Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment