Viongozi wa Serikali ya mtaa wa Katoro wakishirikiana na wananchi wameshiriki zoezi la uwekaji matuta katika baadhi ya barabara za mitaa kutokana na kuwepo kwa ajali nyingi zinazohusisha watoto wa shule kugongwa na magari.
wakizungumza na storm habari baadhi ya wakazi walioshiriki zoezi hilo wamesema kuwa sababu kubwa iliyopelekaea kuweka matuta hayo ni kutokana na kuwepo kwa ajali ambazo zinahusisha watoto wadogo wa shule kugongwa na vyombo mbalimbali vya moto.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kata hiyo Bw.Japheti Madoshi amesema kuwa baada ya kutengenezwa kwa barabara kubwa ya mtaa kumeonekana kuwa na mwendo kasi kwa vyombo vya moto hali ambayo imepelekea kuashiria hatari kwa watembea kwa miguu
No comments:
Post a Comment