Idara ya ardhi mkoani Geita, imelalamikiwa na wananchi wa,mtaa wa shilabela kwa kushindwa kufanya vipimo kwa wakati katika makazi ya wananchi hali ambayo , imesababisha huduma nyingi za kijamii kusimama ikiwemo kutokupatiwa mikopo kutokana na kukoswa hati za nyumba.
Hayo yamebainishwa leo na wakazi wa mtaa huo, walipokuwa wakizungumza na storm habari ambapo wamesema wanaiomba serikali kuchukua hatua za haraka juu ya jambo hilo kwani baadhi yao wamekuwa wakishindwa kupata huduma hizo kutokana na ujenzi holela uliopo mtaani hapo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo bw, Elias Mtoni amesema kuwa suala hilo limekuwa likisababisha msuguano mkubwa baina ya uongozi wa mtaa na idara ya usafishaji mazingira kutokana na kukosekana kwa barabara za kupitishia magari ya taka.
Aidha afisa mipango miji wa halmashauri ya mji wa Geita Kasian Osward ambapo amedai kuwa maeneo yote ambayo hayajapimwa ni vyema kwa wananchi kukaa na viongozi wao ili kuweka makubaliano juu ya hasara ambazo zinaweza kujitokeza katika suala la upimaji wa viwanja.
No comments:
Post a Comment