Wananchi wa kata ya Matendo , mkoani na wilayani Kigoma
wamelalamikia huduma zisizoridhisha za afya zinazotolewazo na zahanati ya kata hiyo,
hivyo wamemwomba diwani kushughulikia kero hizo.
Wananchi hao wametoa malalamiko yao katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mayange, ambapo wamesema
huduma zisizoridhisha zimekuwepo
kwa muda mrefu huku akina mama wakiwa ni wahanga wakubwa wakati
wa kupata matibabu.
Mbali na changamoto
za afya pia wananchi hao wamehoji matumizi mabaya ya fedha za wananchi
ambapo wameeleza zaidi kero zao.
Akijibu kero
hizo diwani wa kata ya Matendo, Athumani Ntanyagara, amesema kuwa
wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana, aliahidi kuwa atasimamia shughuli
zote za miradi ya maendeleo na kulinda
haki za wananchi wa kata hiyo.
Katika hatua nyingine amewahakikishia wananchi
kufuatilia sakata la ubadhirifu
wa fedha lililoibuliwa kwenye
mkutano huo.
No comments:
Post a Comment