Watanzania watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi
Mkoani Tanga wakituhumiwa kuendesha biashara ya kuwasafirisha kwa kutumia
gari aina ya hiace wahamiaji haramu 10 kutoka nchini Ethiopia.
Kamanda wa Polisi Mkoani
Tanga ,Leonard Paulo amesema leo kuwa watanzania hao pamoja
nawahabeshi wamekamatwa jana saa 2.30 usiku katika eneo la Misajini
barabara kuu ya Hedaru- Mombo.
Amesema kuwa wahamiaji hao
walimatwa wakati askari wakiwa doria waliokuwa wakisafirishwa kwenye gari
aina Toyota Hiace iliyokuwa ikiendeshwa na Ally Juma (24) mkazi wa Dar es
Salaam wakiingia mkoani hapa.
Amewataja watanzania wengine
wawili ambao wamekamatwa wakituhumiwa kuwakisafirisha wahamiaji haramu hao
kuwa ni Joseph John (42) mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Iddi Juma(38)
mkazi wa mkoani Iringa.
Ametaja majina ya Wahabeshi
waliokuwa wakisafirishwa kuwa ni
Tarfa Wolder (21),Aramei Yonas (21),Gazae Edson(20),Yohanes Abakar (27),Anemo Tamire (16),Indira Yaiso(18),Wasifimu Paresa (15),Dedacho Gadam (20),Tamelata Abala (17) na Mlatu Shugute (32).
Tarfa Wolder (21),Aramei Yonas (21),Gazae Edson(20),Yohanes Abakar (27),Anemo Tamire (16),Indira Yaiso(18),Wasifimu Paresa (15),Dedacho Gadam (20),Tamelata Abala (17) na Mlatu Shugute (32).
No comments:
Post a Comment