Wananchi wa mtaa wa Jimboni katika kata ya Kalangalala mkoani hapa wamemlalamikia mkandarasi wa Jasco kwa kushindwa kumaliza ujenzi wa barabara hali ambayo imesababisha maji mengi kujaa katika maeneo yao na kusababisha mafuriko.
wakizungumza na Storm habari wananchi hao walisema kuwa usiku wa kuamikia siku ya leo ambapo mvua imenyesha kwa muda mrefu imesababisha athari za maji mengi kuingia maeneo wanayoishi kutokana na kukosekana kwa mitaro katika barabara hiyo.
Walitaja hasara walizozipata ni pamoja na vitu vingi hususani vya umeme kuharibika pamoja na kushindwa kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa kutokana na namna na jinsi hali ilivyokuwa siku ya leo.
Aidha Storm habari ilifanikiwa kumpata mkandarasi wa kampuni hiyo,Bw.Maulid Abdalla,amesema kuwa tatizo hilo wameliona na kwasasa wanalishughulikia na wamekwisha kuagiza watu waende kuchimba mitaro katika maeneo ambayo kumetokewa na tatizo.
No comments:
Post a Comment