Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-05-06

SERIKALI IMEOMBWA KUIPA KIPAUMBELE BAJETI YA BARABARA KATIKA MIKOA YA SIMIYU,KATAVI,GEITA NA SONGWE


Katika kuhakikisha mikoa ya Simiyu, Katavi, Geita, Njombe na Songwe inaondokana na matatizo ya miundombinu serikali  imeombwa  kuipa kipaumbele  cha bajeti mikoa hiyo ili kuweza kutatua chanagamoto hiyo.

Akiuliza swali la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu bungeni dk. Raphaeli Masunga mbunge wa Busega ambapo  amesema, je serikali haioni kuwa kuna haja sasa kwa mikoa mipya na wilaya zingine kupewa kipaumbele cha bajeti ili zipate mafungu ya kutosha.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano mhandisi Edwini Ngonyani amezitaka bodi ya barabara nchini pamoja na Tanroads kuzingatia mahitaji mahususi yaliyoko katika mikoa hiyo pamoja na mikoa mingine ambayo ina mazingira magumu ya usafiri.

Hata hivyo mhandisi  Ngonyani  amesema  kuwa hadi kufikia june 2016 fedha zote za mfuko wa barabara zilizopangwa kugharamia kazi za matengenezo na ukarabati wa barabara zitakuwa zimepokelewa na kupelekwa kwa mawakala wa barabara.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina