Ajali imetokea jana majira ya saa tano za Asubuhi katika eneo la Rukilini, Wilayani na Mkoani Geita na kusababisha watu 15 kujeruhiwa huku mtu mmoja akipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu
Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Hiace yenye nambari za usajili T 859 BFC lililokuwa likitokea mjini Geita kuelekea katika kijiji cha Senga.
Wakielezea namna na jinsi tukio hilo lilivyokuwa baadhi ya majeruhia Bw.Edward Shaban na Kassim Nyombo wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na walipo jaribu kumshauri dereva kupunguza mwendo aliwaambia kuwa anatakiwa kuwahi.
Storm habari ,ilifanikiwa kufika katika hospitali teule ya Mkoa na kuzungumza na Dokta Mahenga Makoye ambae yupo katika kitengo cha dharula na kusema kuwa majira ya saa saba mchana ndipo walipofika majeruhi na wengine walikuwa katika hali mbaya zaidi.
Aidha mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Mkoani hapa Alfred Hussein amesema kuwa hadi sasa wanaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kwamba dereva ametoweka baada ya kusababisha ajali hiyo lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini nini chanzo cha Ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment