SEREKALI imemtaka Dk Mwaka kwenda kwenye sheria kama hajaridhika na uamuzi wa serikali wa kukifungia kituo chake cha tiba za asili.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na wadau wa afya katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.
Ummy alisema kuwa uamuzi uliofanywa na serekali wa kukifunga kituo cha afya cha dk Mwaka ni sahihi kwani hajaonewa kwasababu matangazo na huduma alizokuwa akitoa zilikuwa haziendani na maadili na taratibu za udaktari.
"Dk Mwaka asichonganishe wananchi na serekali yao kwamba tumewafungia huduma walizokuwa wakipata kwake wakati huduma alizokuwa akitoa hazikuwa na sifa"alisema Ummy
Alisema kuwa kama anaona ameonewa aende mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake."Kama anaona tumemuonea aende mahakamani tutakutana huko"alisema
Waziri ummy Mwalimu yupo Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo amezindua jengo la wodi ya wazazi iliyojengwa na shirikala jhpiego lenye thamani ya shilingi milioni 150.
No comments:
Post a Comment