Ingawa kuna taarifa kutoka nchini Zimbabwe zikiarifu kwamba maveterani hao wameamua kutoa waraka wenye kuonesha msimamo wao kwamba kuanzia sasa hawatamuunga mkono tena rais huyo.
Chama hicho kinamshutumu rais Mugabe kwa tabia zake za kidikteta ,kuongoza kwa matakwa yake, na utawala mbovu ,ingawa haijafahamika wazi mpaka sasa ikiwa askari wote wa zamani wamekubaliana juu ya tamko hilo lililotolewa chini ya mwavuli wa chama.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na mkanyiko wa mawazo miongoni mwa wa Zimbabwe kila uchao kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili nchi hiyo kwa sasa.
Kwa sasa rais Robert Mugabe ana mika tisini na miwili,na kwa baadhi ya vikundi wakati fulani ndani ya uongozi wa chama cha Zanu-PF chama wamehusika katika mfululizo wa mapambano kama hayo ili kuinusuru Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment