Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-07-18

YANGA NA AZAM AGOSTI 17 NGAO YA JAMII, SIMBA KUFUNGUA DIMBA NA NDANDA LIGI KUU


MABINGWA wa mataji yote nchini, Yanga SC watamenyana na washindi wa pili wa mashindano yote, Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyovuja   Yanga watafungua dimba na JKT Ruvu Agosti 31 Uwanja wa Taifa.
Kwa ujumla Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/ 2017 itaanza Agosti 20, Simba SC wakifungua dimba na Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi nyingine za ufunguzi zitakuwa kati ya Kagera Sugar na Mbeya City Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Toto Africans na Mwadui FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United na Mbao FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Majimaji na Prisons Uwanja wa Majimaji Songea.  

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina