Mtu
mmoja ameuawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana katika eneo la mtaa wa
Miti mirefu wilaya na mkoa wa Geita.
Tukio hilo limetokea majira ya usiku wa
kuamkia leo ambapo marehemu aliyefahamika kwa jina la Lucas Dagadaga 65 mkazi
wa kijiji cha Mbabane, ambaye alikuwa ni mlinzi wa maduka ya mtaa huo, ameuawa
kwa kupigwa na kitu kizito kichwani akiwa katika eneo la lindo lake.
Storm habari imefika katika eneo la tukio na
kuzungumza na baadhi ya mashuhuda ambapo wamesema kuwa suala la mauaji mkoani
hapa limekuwa likijitokeza mara kwa mara huku wakililalamikia jeshi la polisi
kushindwa kuchukua hatua dhidi ya matukio yanayokuwa yakijitokeza kwani tukio
la kuuawa kwa walizi sio la kwanza.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa baada ya mauaji hayo
watuhumiwa walivunja duka la Adinani Dauda 36 mfanyabiashara wa eneo hilo na
kupora fedha kiasi cha shilingi 800,000,
vocha mbalimbali zenye thamani ya tsh 100,000 sambamba na simu 7 za wateja
zilizokuwa zikichajiwa dukani hapo ambapo wamiliki na thamani yake bado
hazijaweza kufahamika.
Aidha kamanda Mponjoli ametoa wito kwa waajiri kuacha tabia ya kupenda vitu rahisi
kwa kuajiri walinzi wasiokuwa na viwango na badala yake kuhakikisha wanaajiri
watu walio na viwango vya ulinzi ili
kuepusha maujai hayo.
No comments:
Post a Comment