Watu 3 wamegunduliwa wakiwa wamefariki huku
baadhi ya sehemu za miili yao kuliwa na wanyama katika eneo la mlima
Kitongo wilaya ya Nyangwhale mkoani Geita.
Tukio hilo limegunduliwa august 22 majira ya saa
saba mchana katika kijiji hicho kilichopo katika kata ya Kakora wilaya ya Nyangwhale
mkoani hapa ambapo marehemu hao waliotambulika kwa Leticia Charles 40, Salu
Nyanda 65 na Frola Thomas 2 wote wakiwa ni wakazi wa kijiji hicho wamekutwa
wamefariki umbali wa mita 200 kutoka barabara kuu ya kijiji hicho.
Inadaiwa kuwa kati ya julai 22 na 27 mwaka
huu majira ya saa mbili usiku marehemu waliondoka nyumbani wakidaiwa kuelekea kwa
mganga wa kienyeji aitwaye Ndutu Maswila 65 mkazi wa kijiji cha Nyangalamila
kwa ajili ya kupata tiba na tangu hapo
hawakuonekana tena hadi walipogunduliwa wakiwa wamefariki na baadhi ya miili
yao kuliwa na wanyama.
Aidha katika eneo la tukio zimekutwa nguo
zilizotambuliwa kuwa ni za marehemu hao , sufuria mbili zikiwa kwenye mafiga huku
ndani kukiwemo dawa za miti shamba huku pembeni kukiwa na mafuvu mawili.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema jeshi la polisi linaendelea
na upelelezi ili kubaini kiini cha tukio na baadae kuwakamata wahusika wa tukio
hilo.
No comments:
Post a Comment