Uchaguzi Mkuu wa marudio wa
Zanzibar umefanyika kwa amani na utulivu huku kukiwa na idadi ndogo ya wapiga
kura, ikilinganishwa na idadi ya waliojitokeza katika uchaguzi uliofutwa wa
Oktoba 25, mwaka jana.
Takwimu za Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC), zinaonyesha kuwa waliojiandikisha kwenye Daftari la
wapiga kura kwa Unguja na Pemba ni 503,860, na sehemu zote hizo zilikuwa na
jumla ya vituo vya kupigia kura 1,580, na kila kituo kina wastani wa
wapiga kura 350.
Katika uchaguzi huo
vyama vya CCM, AFP, ADC na CCK vimeshiriki katika uchaguzi huo na
kuweka mawakala wake vituoni huku chama cha CUF kikiwa hakina wakala yeyote
kwenye vituo vyote vya kupiga kura vya kisiwani Unguja.
Pamoja na kuwepo kwa hali ya
taharuki katika siku za karibuni visiwani hapa, hali hiyo imekuwa tofauti
ambapo leo maeneo mengi yalionekana kuwa na amani, pia vikosi vya ulinzi
havikujitokeza barabarani kama ilivyozoeleka.
Maduka mengi
yalionekana kufungwa na katika vituo vya kupiga kura ambavyo inadaiwa ni
ngome ya CUF, watu walijitokeza kwa idadi ndogo ikilinganishwa na wale
waliojitokeza kwenye maeneo ambayo ni ngome ya CCM.
Katika Kituo
cha Shule ya Sekondari Bububu pamoja na msimamizi wa kituo hicho Mohammed
Zamani, kusema kuwa watu walijitokeza kwa wingi kupiga kura, wakala wa
chama cha AFP, Fumo Machano Fumo alieleza kuwa tokea kufunguliwa kwa kituo hadi
sita mchana watu waliokuwa wamepiga kura katika chumba chake walikuwa 25.
No comments:
Post a Comment