Hivi ndivyo Chidi Benz anavyoonekana kwa sasa. |
Katika
mitandao ya kijamii Jumamosi iliyopita kulisambaa picha za rapa Chidi Benz
ambazo zinamuonyesha jinsi alivyokonda na kupoteza ule mwili wake wa kuvutia
aliokuwa nao zamani.
Mkali huyo wa wimbo Dar es Salaam Stand
Up, anakubalika na vijana wengi kutokana na uwezo wake wa kuandika pamoja na
kuchana. Lakini miaka ya hivi karibuni alianza kubadilika baada ya kujiingiza
kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Oktoba 24 mwaka 2014, Chidi alikamatwa
na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere wakati akielekea
jijini Mbeya kwa ajili ya show. Lakini kesi hiyo ilimalizika miezi michache
baadaye baada ya kuamriwa na mahakama kulipa faini.
Tukio hilo liliwafanya wasanii
mbalimbali kuzungumzia hali hiyo huku wakimshauri kuachana na matumizi ya madawa
ya kulevya. Ray C ambaye ni mmoja kati ya waathirika janga hilo ambaye kwa sasa
yupo kwenye tiba ya methadone, aliamua kumshauri Chid Benz.
“Pole
kaka yangu Chidi Benz. Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitafutia
jibu la kutatua tatizo lako. Mimi ni dada yako natumeshafanya kazi pamoja,
tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu
nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake
ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani,” aliandika Ray C
kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo Chidi Benz aliendelea na
harakati zake huku akijinadi katika vyombo vya bahari kwamba tayari
ameshaachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Lakini watu wake wa karibu
pamoja na marafiki zake walikuwa wanadai kwamba bado hajaacha.
Lakini Jumamosi hii akiwa katika kipindi cha Da Weekend Chart Show cha Clouds TV, Chidi amelionekana amechoka zaidi huku akiowamba wadau mbalimbali kumsaidia.
“Matatizo
yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua
kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.
Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki
wa Hip Hop, Afande Selle, alionyesha kusikitishwa na jinsi madawa ya kulevya
yanavyomaliza nguvu kazi ya taifa.
“Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mitaaani kote mitaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleoooo,madawa ya kulevya yanaua masela leooooo,”alisema Afande Selle.
“Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mitaaani kote mitaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleoooo,madawa ya kulevya yanaua masela leooooo,”alisema Afande Selle.
Pia wadau mbalimbali wamewataka watu
pamoja na wasanii wenzake kumsaidia huku Arnold Kayanda, mtangazaji wa BBC
Swahili akisema amelipokea kwa masikitiko suala hilo.
“Kama picha hii ni rafiki yangu Chidi
Benz kama nilivyotaarifiwa, kwa hisani yenu wote naomba kila mtu kwa nafasi
yake amsaidie. Mimi niko mbali lakini nikirudi nitakutana naye,” alisema.
Licha
ya wadau mbalimbali kutaka asaidiwe lakini bado tunaona hakuna msaada wa haraka
ambao mpaka sasa umechukuliwa ili kumuokoa Chidi Benz.
Serikali ya Magufuli ni sikivu sana, bila shaka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijana mpenda sanaa, Nape Moses Nnauye ataliangalia suala hili.
Serikali ya Magufuli ni sikivu sana, bila shaka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijana mpenda sanaa, Nape Moses Nnauye ataliangalia suala hili.
No comments:
Post a Comment