Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) mkoani Geita inamshikilia bw,Shukurani Kulwa Musa,kwa kufanya kazi ya uuguzi bila ya kuwa na sifa ambazo zinamruhusu kufanya kazi hiyo.
Akizungumza na Storm habari mkuu wa takukuru mkoani hapa,Thobias Ndaro, amesema kuwa taarifa za kupatikana kwa daktari huyo walizipata wiki moja kabla ya ujio wa waziri mkuu na baada ya kufanya uchunguzi wa kina ulioweza kubaini kuwa bw,Shukurani hakuwa na sifa za kuwa daktari hali ambayo ilipelekea kumkamata kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Ndaro ameeleza kuwa kwa mjibu wa uchunguzi ambao wameufanya walibaini kuwa daktari huyo ni wale watu ambao wanafanya mazoezi ya vitendo na kwamba kwa sasa bado wanaendelea na uchunguzi zaidi na utakapo kamilika watatoa taarifa kamili juu ya daktari huyo.
AidhaStorm habari ilifanikiwa kufika katika ofisi za mkurugenzi na kukutana na kaimu mkurugenzi wa halamshauri ya wilaya,mwalimu Deus Self,ambapo amesema kuwa ni kweli alipatiwa taarifa za mganga huyo ambae ni feki lakini kwa madai ambayo mganga huyo alikuwa nayo alidai kuwa anajitolea katika hosptali hiyo.
No comments:
Post a Comment