Madereva wa vyombo vya moto mkoani Geita wameshauriwa kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria za barabarani ili kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara na kusababisha vifo vya watanzania wengi.
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa mkuu wa kitengo cha usalama barabarani (RTO) mkoani hapa,sajenti Deus Mgema,wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya usalama barabarani yanayotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Greenmood Organization.
Amesema kuwa ni vyema kwa dereva anapokuwa barabarani kuwa na nidhamu pindi anapokuwa akiendesha chombo cha moto ikiwa ni pamoja na kufata kanuni za usalama.
Kwa upande wake,bw Falesi Lujoja,amesema kuwa ni vyema kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye mafunzo hayo kutilia maanani kile wanachofundishwa.
Aidha mkurugenzi wa taasisi hiyo,Daniel Makungu,ameeleza dhumuni la kufungua taasisi hiyo ni kuhakikisha kila mtu anayetumia barabara anarudi akiwa salama nyumbani na kudhibiti ajali za mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment