Gari aina ya fuso yenye namba za usajili T-939bnz ambalo linafanya kazi za ubebaji wa mawe, limemgonga bw, Emanuel Kang’wena mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Katoro katika njia panda ya kijiji cha Inyara wilayani na mkoani Geita na kumsababishia kifo.
Akithibitisha kupokea mwili huo kaimu mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Katoro bw,Bahati Machaguli amesema kuwa sababu iliyo pelekea kifo chake ni kutokwa na damu nyingi eneo la kichwa
Aidha baadhi ya mashhuda walioshuhudia tukio hilo wameieleza storm habari kuwa marehemu alitaka kupanda gari hilo wakati likiwa kwenye mwendo ndipo alipo teleza na kuangukia katika uvungu wa gari hilo na ndipo lilipo mgonga na kufariki papo hapo
No comments:
Post a Comment