Kufanya kazi Ulaya ni
raha sana kwa maana ya kupiga hatua, lakini nako kuna ugumu wake kimaslahi kama
utalifikiria suala la kodi.
Najua unatamani kujua
maisha ya wanasoka wa Ubelgiji hususani
katika kipindi hiki anachocheza soka mtanzania Mbwana Samatta nchini
humo,
Kwa mujibu wa mtandao
wa www.xpats.com hadi kufikia April 10 2015 mishahara ya
wachezaji wengi wa Ligi Kuu Ubelgiji ilikuwa inatajwa kuwa ya
wastani wa euro 253,586 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya milioni 600 za
kitanzania kabla ya kukatwa kodi pamoja na bima.
Mshambuliaji mpya wa KRC
Genk, Mbwana Samatta atakuwa akilipwa mshahara wa euro 35,600 (zaidi ya Sh
milioni 85) kwa mwezi.
Lakini makato ya kodi,
kupitia kwa Mamlaka ya Kodi ya Ubelgiji, yanamfanya Samatta kuondoka na kiasi
kidogo tu cha kodi.
Taarifa za uhakika
kutoka Ubelgiji zinasema, Samatta atakuwa akikatwa asilimia 48 kama utajumlisha
‘TRA ya huko’ na makato ya mshahara ya serikali ya mshahara wake. makato ambayo
wanakumbana nayo wageni wengi wanaofanya kazi nchini humo.
Pamoja na kulipwa zaidi
ya Sh milioni 85, maana yake Samatta atakuwa akipokea euri 18,200 (zaidi ya Sh
38,584).
kabla ya kutua KRC Genk,
alikuwa akipokea kitita cha dola 15,000 (zaidi ya Sh milioni 32) kutoka kwa TP
Mazembe ambayo aliitumia vizuri kujitangaza.
Maana yake kwa mshahara
atakaokuwa akichukua Samatta inaonekana hakuna tofauti kubwa sana na ule
aliokuwa akichukua TP Mazembe.
Lakini inawezekana
alichoangalia zaidi ni suala la hatua kwa ajili ya kupata mafanikio zaidi hapo
baadaye kimshahara pia kiuchezaji kwa ajili ya kutimiza ndoto zake.
Kwa mwezi huwa inatajwa
kufikia wastani wa euro 20000 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania.
Klabu ya Anderlecht iliyopo nafasi ya tatu katika Ligi, ndio inatajwa
kuwa klabu inayolipa mishahara mikubwa zaidi, kwa mwaka Anderlecht inalipa
hadi euro 600000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.4 za kitanzania kwa
mchezaji mmoja.
Klabu ya KRC
Genk anayocheza nahodha wa Taifa Stars Mbwana
Samatta inatajwa kuwa miongoni mwa vilabu tajiri ndani ya Ligi
Kuu Ubelgiji, ila kwa mujibu wa www.xpats.com, wachezaji wengi
wao Ubelgiji hulipwa kati ya euro 25000 hadi 50000 kwa mwezi.
KWa sasa, Samatta ni mwanamichezo anayeshika
nafasi ya pili kwa kulipwa mshahara mkubwa nyuma ya Hasheem Thabeet ambaye
alikuwa akichukua mshahara hadi dola 200,000 kwa mwezi wakati akikipiga ndani
ya NBA na sasa hata kama amepunguziwa kwa kuwa yuko ligi ya chini, haiwezi kuwa
chini ya dola 100,000 kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment