Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
amesema Jiji la Dar es Salaam litafumuliwa na kupangwa upya baada ya Ramani ya
Mipango Miji (Master Plan) mpya kukamilika.
Pia, amesema Serikali ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha ndani ya
miaka 10 ijayo, ardhi yote nchini itakuwa imekamilika kupimwa na kupangwa kwa
matumizi mbalimbali.
Akizungumza na wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi Dar es
Salaam jana, Waziri Lukuvi alisema Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa ubovu
wa upangaji miji.
Alisema kwa sababu hiyo, ameagiza kuandaliwa kwa Mpango Mji Mpya
ambao utakamilika Julai, baada ya ule wa awali kuoneakana mbovu.
“Mwanzo hatukufanya vizuri. Tuliajiri Consultant (mshauri) wa
Master Plan (Mipango Miji) kutoka Italia sitaki kumtaja na yule Mswahili na
wengine walioshirikiana nao, lakini kwa ufupi walifanya vibaya. Fedha imekwisha
lakini kazi siyo nzuri,” alisema.
No comments:
Post a Comment