Hotel ya Luns iliyopo maeneo ya mtaa wa Miti Mirefu kata ya Kalangalala imenusurika kuungua kwa moto kutokana na hitilafu ya umeme ambayo ilikuwa imetokea katika nguzo ya mita.
Wakizungumza na Storm habari baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamesema kuwa hitilafu iliyotokea katika hotel hiyo imesababishwa na Transfoma , ambayo imewekwa katika mtaa huo kwani si mara ya kwanza kwakutokea kwa hitilafu ni mara kwa mara tatizo limekuwa likijitokeza.
Hata hivyo kwa upande wake,Christina Sunga ambae ni kamanda wa zima moto, amesema kuwa taarifa walizipata kwa wananchi kwa kupigiwa simu na waliweza kufika kwa wakati na kufanikisha kuuzima moto huo.
Kutokana na lawama nyingi kuelekezewa katika shirika la umeme tanesko mkoani hapa,Storm habari imefanikiwa kufika katika ofisi za shirika hilo na kuzungumza na ,mwandisi wa shirika hilo ,Ndemba William,ambapo amesema kuwa chanzo cha moto huo ilikuwa ni hitilafu ambayo ilianzia katika waya unaoingiza umeme katika hotel hiyo.
No comments:
Post a Comment