
Wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wamempongeza
Rais John Magufuli kwa hatua aliyochukua ya kuahirisha maadhimisho ya siku ya
Muungano na kuokoa zaidi ya Sh bilioni mbili na kuagiza fedha hizo zitumike
kufanya upanuzi wa Barabara ya Ghana kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Pamoja na pongezi hizo, wamemuomba Rais Magufuli baada ya
barabara hiyo kukamilika kufanyiwa upanuzi, ipewe jina la “Barabara ya
Muungano” kama njia ya kuienzi kauli yake hiyo aliyoitoa kwa wakazi wa jiji
hilo.
Rais Magufuli akiwa Chato mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko,
juzi alitangaza kuahirisha maadhimisho ya siku ya Muungano mwaka huu na kuagiza
fedha ambazo zingetumika kwa vinywaji, halaiki, gwaride na vyakula ambazo ni
zaidi ya Sh bilioni mbili, zitumike kufanya upanuzi wa Barabara ya Ghana –
Airport.
Kadhalika alielekeza siku hiyo iwe siku ya mapumziko ya kawaida
kwa Watanzania kuiadhimisha wakiwa katika shughuli zao binafsi.
No comments:
Post a Comment