Wananchi mkoani Geita wamelalamikia suala la wafanyabiashara wa sukari kupandisha gharama kutoka katika bei ya shilingi 2000 hadi kufikia shilingi 2500 hali ambayo imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa wananchi wenye vipato vya chini.
Wakizungumza na Storm habari wananchi hao wamesema kuwa suala hilo limekuwa likiwapa changamoto kubwa kwani kutokana na kushindwa kununua sukari ambayo imekuwa ikipanda siku hadi siku .
Aidha wafanyabiashara mkoani hapa wamesema kuwa suala hilo limesababishwa na upatikanaji wa bidhaa kuwa ghali huku wengine wakidai kuwa ni kutokana na kuzuiliwa uingiaji kwa sukari iliyokuwa ikitokea nje ya nchi.
Kutokana na hali ya sukari kuwa juu wafanyabiashara wameiomba serikali kuruhusu sukari ya nje kuingizwa nchini jambo ambalo litasaidia kupunguza adha na uhaba wa sukari.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Magufuli february 18 alipokutana na makundi mbalimbali yaliyoshiriki katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015
wakiwemo wasanii alipiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kulinda na kuviendeleza viwanda vya hapa nchini.
No comments:
Post a Comment