Wananchi wa mtaa wa Mwembeni kata ya Nyankumbuku mkoani Geita wameendelea kusisitiza kuwa hawataondoka katika maeneo ambayo yanasemekana kuwa ni ya jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi kutokana na kwamba maeneo hayo wana uhalali wa kuyamiliki.
Wakizungumza mbele ya diwani wa kata ya Nyankumbu katika mkutano wa kujadili hatma ya maeneo ambayo waliambiwa na mkuu wa wilaya ya Geita, Mh Manzie Manguchie kuyaachia na kuacha kufanya shughuli yoyote.
Wamesema kuwa jumuhiya ya wazazi,waliwaruhusu mbele ya mahakama kuwa waendelee na shughuli zao sababu ya kukosekana fedha za kuwafidishia,swala ambalo liliwapa wasi wasi ni baada ya mkuu wa wilaya kuwataka kuondoka maeneo hayo kwa madai kuwa si maeneo yao ni ya jumuhiya hiyo.
Diwani wa kata ya nyankumbu michael kapaya amesema kuwa swala hilo lipo kinyume na makubaliana kutokana na kwamba vielelezo vipo na vinaonesha kuwa jumhiya hiyo ilishindwa gharama na kwamba hawatakubaliana na hatua ambayo inataka kuchukuliwa kwa kuwaondoa wananchi maeneo yao.
Aidha,mkuu wa wilaya ya Geita Manguchie amesema kuwa tatizo lililopo katika eneo hilo ni uwelewa na kwamba wanatakiwa kujua kuwa kabla ya kutaka kujenga ni vyema wakapata kibali cha ujenzi na kwamba juu ya eneo hilo kuna hati ya ardhi ambayo inawatambua wamiliki ni jumuhiya ya wazazi.
No comments:
Post a Comment