Wananchi wa mji mdogo wa Katoro wilayani Geita, wameendelea kuishukuru kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu (GGM),kwa kutoa msaada wa matibabu kwa waathirika wa midomo sungura.
Storm habari imezungumza na baadhi ya wazazi ambao walikuwa na watoto wenye tatizo hilo,ambapo wamesema kuwa kabla ya kupatiwa msaada wa upasuaji wa watoto wao hali ilikuwa ni tofauti kutokana na kukosa gharama za matibabu.
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Katoro, Peter Janga amesema tatizo hilo ni kubwa katika mkoa wa Geita, na hali hiyo inaonekana kukithiri kutokana na kwamba kila mwezi huwa wanapokea takribani watoto watatu.
Theophil Pima ambae ni Afisa Mawasiliano mwandamizi wa mgodi huo,amesema toka mwaka 2001 hadi hivi sasa kampuni ya GGM imegharamia matibabu takribani wagonjwa 700,na zoezi hili ni endelevu kutokana na kaulimbiu yao ya jamii inayozunguka mgodi lazima ifaidike na uwepo wa mgodi huo.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali Afisa habari halmashauri ya wilaya ya Geita Bi.Trovina Kikoti amesema kuwa serikali inatoa shukrani za dhati kwa GGM,kwa kutoa msaada wao kwa ajili ya matibabu pia ameishauri jamii isiwafiche watoto ndani wenye matatizo hayo kwani yanatibika
No comments:
Post a Comment