Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella (pichani) ametoa saa 24 kwa
kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi
kuipata komputa iliyoibiwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba
kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uaandaji wa malipo ya
Halmashauri (EPICOR)
Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye
kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo
taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye
chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya
halmashauri.
“OCD kesho nitakwenda
kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu,
vinginevyo hatutaelewana",amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza
kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.
Akizungumza kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri, kaimu
mhazini wa halmashauri hiyo Baraka Munuo, alidai kupokea taarifa za kupotea kwa
Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe
akimuelezea upotevu huo.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe,, kupitia mafaili na
kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo
ambalo mkuu wa mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.
”Mkurugenzi nakuagiza
pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda
mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie
kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili
yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo
kingine.
Awali akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe
Joseph Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni
shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema wilaya
imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa kimepiga kambi
katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.
Mkuu wa mkoa wa yupo katika ziara yakujitambulisha na hii ikiwa
ni wilaya yake ya saba,Mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi, Magu,
Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe inakuwa wilaya ya saba huku
akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye halmashauri za Buchosa na
Sengerema yenyewe.
No comments:
Post a Comment