Serikali imekiri kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa watu katika magereza huku sababu ikielezwa ni ucheleweshwaji wa kesi unaosababishwa na kucheleweshwa kwa kesi za baadhi ya washitakiwa.
Akizungumza na watendaji wa Serikali mkoani Geita katika ofisi za mkuu wa mkoa,Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Herson Mwakyembe amesema kuwa kutokana na kucheleweshwa kwa kesi hali hiyo imekuwa ikisababisha kuwepo kwa mlundikanao mkubwa wa watu hali ambayo imeendelea kutishia usalama wa afya kwa baadhi ya wafungwa.
Akitoa taarifa ya Wkoa kwa Waziri Mwakyembe Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mh.Manzie Manguchie amesema kuwa mkoa wa Geita unakabiliwa na uhaba wa gereza la mkoa hali ambayo kumekuwa na changamoto ya watu kuwa wengi katika magereza.
Aidha waziri Mwakyembe amewata wananchi mkoani hapa kubadilika na kuachana na vitendo vya imani za kishirikina za mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (zeruzeru) huku akiitaja mikoa ya Mwanza,Mara na Geita kuongoza kwa mauaji hayo.
Waziri Mwakyembe amefika asubuhi na mapema leo akitokea jijini Mwanza na yupo mkoani Geita kwa ziara ya siku moja ambapo atatembelea,Ofisi ya Mwanasheria mkuu,Ofisi ya vizazi na vifo (RITA) na kuzungumza na wafungwa katika gereza la wilaya ya Geita.
No comments:
Post a Comment