Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-04-17

DC AAGIZA KUSAKWA ALIYEMPA MIMBA MWANAFUNZI

Image result for mkuu wa mkoa kagera

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Jackson Msome ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kumsaka na kumtia mbaroni kisha kumfikisha mahakamani mtu aliyempa mimba mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Karabagaine iliyoko wilayani humo.


Msome alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipofanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo na kupewa taarifa kuwa mwanafunzi huyo ni mjamzito.

“Vyombo vya ulinzi na usalama kaeni na mwanafunzi huyo anamtambua aliyempa mimba, mhoji na hakikisheni mnamkamata mtu huyo kisha afikishwe mahakamani kujibu tuhuma hiyo,” alisema na kuongeza: “Pia jamii fichueni wale wanaowapa mimba watoto wetu wa kike, wanaowaoa na kuwaozesha waweze kutiwa mbaroni na kupambana na mkono wa sheria.”

Alisema kutokana na tabia hizo, watu wawili wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwapa wanafunzi mimba katika shule za sekondari za Nyakibimbili ambako wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza, Alicia Vedasto na Dominatha Jacob wamepewa ujauzito.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina