Wananchi waishio mtaa wa Mgusu wilayani na mkoani Geita wametakiwa kujua kuwa wanaishi katika sehemu ya leseni ya utafiti wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita( GGM) na kwamba eneo hilo bado mgodi haujaona sababu ya kulichukua.
Akiuliza swali katika kipindi cha maswali na majibu Mbunge wa viti maalum CHADEMA mkoani hapa Upendo Peneza, ametaka kujua kuwa serikali inaweka msukumo gani kwa mgodi kuhakikisha kuwa inawalipa wananchi fidia ili waweze kuondoka katika maeneo hayo.
Akijibu swali la mbunge wa viti maalum,mkoani hapa Naibu Waziri wa nishati na madini Dkt.Merdad Kalemani amesema kuwa kwa sasa hivi eneo hilo bado halijaanza kutumika na kwamba mgodi hauoni sababu ya kulichukua .
Katika hatua nyingine pia wananchi mkoani hapa wamekuwa na maoni tofauti juu ya bunge la bajeti ya mwaka 2016/17 lililoanza rasimi hii leo mkoani dodoma.
No comments:
Post a Comment