Baraza la madiwani wa halamshauri ya wilaya ya Geita limemsimamisha kazi mhandisi wa halmashauri hiyo Mathiasi Shoto,kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi ikiwa ni pamoja na kushindwa kutaja barabara ambazo amekwishakamilisha tangu alipokabidhiwa uongozi huo.
Kwa upande wao madiwani wa halmashauri hiyo wamesema kuwa kusimamishwa kazi kwa mhandisi huyo kutatoa changamoto kwa watendaji wengine kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika jamii.
Hata hivyo kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Geita,mh Manzie Manguchie ambaye alikuwepo katika kikao hicho amewataka watumishi wa serikali kuwa waamianifu na waadilifu huku akiwataka pia kuacha udanganyifu katika shughuli zao.
No comments:
Post a Comment