Mtu mmoja ambaye ni mlinzi wa kampuni ya Massa security,ameuawa na watu wasio julikana,kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali usoni kwenye ofisi za voda shop zilizopo eneo la stendi mpya mkoani Geita baada ya kuvamiwa na majambazi usiku wa kuamkia jumatano.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina msaidizi wa polisi mkoani hapa,mponjoli mwabulambo amesema kuwa tukio hilo, limetokea majira ya saa tisa na nusu usiku na polisi walipomchunguza walibaini kuwa alikuwa ameshambuliwa na kitu chenye ncha kali usoni.
Majambazi hao baada ya kufanya mauaji hayo walifanikiwa kuvunja mlango wa voda shop hiyo na kupora simu 7 aina ya smart phone na tablet.
wakizungumza na storm habari katika zoezi la kumwaga Athumani Mujombi aliyekuwa akifanya shughuli za ulinzi kwenye kapuni hiyo baadhi ya asikari wa kampuni hiyo wamesema kuwa Kutokana na matukio ya kuuwawa kuongezeka mkoani Geita, hali hiyo imepelekea baadhi ya walinzi kuwa na uoga hali ambayo inasababishwakutokuwa na uhakika wa maisha yao pindi wanapokuwa katika malindo huku wakiiomba serikali kusimama kidete ili kutkomeza hali hiyo.
Bw Azizi Abduli ambae pia ni mlinzi wa Massa security,amesema kuwa wanasikitishwa pia na baadhi ya wamiliki wa kampuni za ulinzi kwa kuendelea kuwa kandamiza kwani wamekuwa wakinyimwa likizo pamoja na kutokupewa huduma za kiafya ikiwa ni pamoja na kuingizwa katika mifuko ya hifadhi ya taifa.
Kwa upande wake meneja wa kampuni hiyo bw, ,Reymond Sweki,ameeleza kuwa tukio hilo limekuwa ni tukio la 3 kutokea ndani ya kampuni hiyo ambapo, askari wanne wameuwawa kikatili katika matukio tofauti kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi june 2016 wakiwa katika shughuli za ulinzi.
No comments:
Post a Comment