Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-07-22

Mourinho adokeza Pogba atatua Man Utd


Jose Mourinho ametoa kidokezo cha karibuni zaidi kwamba Manchester United wanataka kumnunua tena Paul Pogba kutoka Juventus ya Italia.

Mourinho amesema “mmeona moshi, jueni kuna moto”.Pogba


United wanadaiwa kutoa £100m, ambayo ni rekodi ya dunia, kumnunua mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 23.
Pogba aliondoka Old Trafford mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 19.
Manchester United walilipwa £800,000 pekee na klabu hiyo ya Italia.
"Sitawafanya kuwa watu wasiojua na kutaka kuwaonesha kwamba hatujaribu kumnunua mchezaji mmoja,” amesema Mourinho.
Meneja huyo kufikia sasa amenunua wachezaji watatu: beki Eric Bailly kutoka Villarreal, kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund na mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic.
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kumnunua Pogba, Mourinho alisema: “Tulijiwekea malengo matatu, tulipata watatu na tutampata huyo wa nne.”

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina