Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-07-22

Mzozo wazuka kuhusu shamba la Osama Pakistan

Jeshi
Mzozo umezuka nchini Pakistan kuhusu shamba ambapo kiongozi wa zamani wa mtandao wa al-Qaeda Osama bin Laden alikuwa anaishi mjini Abbottabad.

Bin Laden aliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani katika shamba hilo Mei 2011 
Maafisa wa jiji wanataka kugeuza shamba hilo kuwa uwanja wa kuchezea watoto.
.Osama
Hata hivyo, jeshi linataka kipande hicho cha ardhi kigeuzwe na kuwa makaburi.
Kuna baadhi ya wakazi wanaotaka shamba hilo litumiwe kujenga shule ya wasichana huku baadhi ya wanajeshi nao wakitaka ligeuzwe kuwa bustani ya burudani na kutumiwa kuzalisha mapato kwa serikali.
Huku mzozo kuhusu pande hizo mbili ukiendelea, jeshi mnamo Jumatano lilifika na kujenga ua, jambo lililoshangaza maafisa wa baraza la jiji.
Bin Laden aliishi kwenye jumba la ghorofa tatu lililo kwenye shamba hilo bila kujulikana kwa miaka kadha. Jumba hilo lilikuwa limezungushwa ua mrefu.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina