Mahakama kuu kanda maalumu ya Iringa leo imesendelea na kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha cha Channel Ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi, inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Pasificus Cleophace Simon mwenye namba G 2573
Hukumu ya kesi hiyo awali ilipangwa kutolewa July 21 mwaka huu, iliahirishwa hadi leo kutokana na jaji anayesikiliza kesi hiyo kuwa nje ya mkoa kikazi.
Leo July 25 2016 taarifa iliyoripotiwa na kituo cha ITV ni kwamba mahakama kuu Iringa imemtia hatiani kwa kuua bila kukusudia askari huyo na hivyo hukumu rasmi itatolewa siku ya jumatano.
No comments:
Post a Comment