Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-07-25

Zitto Kabwe na Maalim Seif Kutua Marekani kwa Clinton

ZITTO Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad kwa pamoja wameitwa jijini Philadelphia, Marekani.

Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Wanasiasa hao wameitwa kuhudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Demokratiki utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa Marekani kupitia chama hicho.

Marekani inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu tarehe 8 Novemba mwaka huu ambapo Clinton atathibitishwa kwenye mkutano huo kupambana na Donald Trump wa Chama cha Republican.

Maalim Seif na Zitto ndio wanasiasa pekee nchini waliopata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.

Abdallah Khamis, Ofisa Habari wa ACT- Wazalendo amesema wakati Zitto akiwa kwenye mkutano huo, atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani.

Taarifa zinaeleza kuwa, viongozi hao ni wawakilishi wa wanasiasa mahiri kutoka upinzani nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina