Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-07-17

UVCCM wawasaka BAVICHA Dodoma....Waandaa vijana 3000 Kuimarisha Ulinzi


Umoja wa Vijana CCM, wametua mjini Dodoma ambapo Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unatarajiwa kufanyika wiki hii huku wakiwatafuta wajumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) ambao awali walipanga kuzuia kufanyika kwa mkutano huo.

Akiwa katika Ofisi za UVCCM – Dodoma jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefika mjini hapo pamoja na mambo mengine kusimamia ulinzi wa chama na viongozi wa chama hicho lakini hawaoni BAVICHA.

“Nipo hapa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuongoza shughuli za ulinzi wa chama na viongozi wetu, kama Mtendaji Mkuu na mtoa maelezo ya itifaki. Kwa bahati mbaya kwa muda wote sijaona dalili wala harufu ya BAVICHA. Hii inadhihirisha kwamba kusema na kutenda ni vitu tofauti,”alisema Shaka.

Aliongeza kuwa wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya kazi ya kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho tawala.

Aliwahakikishia usalama wajumbe wa Kamati Kuu akiwataka kuwa na amani kwani wataingia na kuondoka mjini humo wakiwa salama.

Juzi, BAVICHA walitangaza kurudi mjini Dododoma kwa lengo la kufanya Mkutano wao wa Kamati ya Kiutendaji baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwataka kusitisha adhma ya kutaka kuzuia kufanyika kwa mkutano wa CCM.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina