Dkt Kigwangala ameyasema hayo mapema hii leo alipofanya
ziara ya siku moja mkoani hapa ya kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa pamoja
na vituo 2 vya afya ambavyo ni kituo cha Nyankumbu na hospitali ya Makoye kwa lengo la
kukagua utendaji kazi katika sekta ya afya.
Amesema kuwa ni vyema sasa vituo vyote vilivyopewa hadhi ya
kuitwa vituo vya afya vikawa na huduma za upasuaji huku
akisisitiza kuwashusha hadhi waganga wa vituo na vituo vyao vitakavyoshindwa
kutoa huduma hiyo hadi katka ngazi ya zahanati.
Akisoma taarifa ya utekelezaji mbele ya naibu waziri mganga mkuu wa mkoa wa Geita dkt Kisala Joseph amesema kuwa serikali inaendelea na ujenzi wa vituo 2 vya afya mkoani hapa vitakavyokuwa vikitoa huduma ya upasuaji ambavyo vitajengwa katika wilaya ya Mbonge na Chato,
Naibu waziri akiwasili mkoani Geita |
Naibu waziri akitoa maagizo kwa watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita |
No comments:
Post a Comment