Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-08-19

Watu wawili wameuawa kwa kuchomwa moto mkoani Geita wakidaiwa kuhusika na uvuvi haramu

GWANGALALAA 1
Miili miwili imechomwa moto katika kijiji cha Nyamalele baada ya kutuhumiwa kuhusika na uvuvi haramu
Watu 2 wameuawa kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wavuvi haramu waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi kwa kutumia sumu katika ziwa victoria na kisha watu hao kubomoa  nyumba ya mrehemu huyo hali ambayo imewalazimu askari kutumia silaha kali ili kuwatawanya watu hao.


Tukio hilo limetokea mnamo majira ya saa kumi usiku wa kuamkia leo katika kjiji cha Nyamalele kata ya Nkome wilayani na mkoani Geita ambapo marehemu mmoja aliyefahamika kwa jina la Franco Mganda 50 mkazi wa kijiji cha Nkome na mwingine ambaye bado jina lake halijajulikana wameuwa na wananchi kisha kuteketezwa kwa moto.

Wakizungumza na mtoto wa jakuba blog baadhi ya mashuhuda waliofika kushuhudia tukio hilo bw Thobias Kapuli na bw Tom Samsoniwamesema kuwamarehemu aliyefahamika kwa jina la franco alikuwa ni mwendesha pikipiki ambaye alikuwa ameenda kubeba samaki wanaodaiwa kuwa walikuwa wamevuliwa kwa njia haramu ndipo akiwa njiani alikutana na watu wasiojulikana wakaanza kuanza kuwashambulia na hatimae kupoza maisha.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Geita mh Herman  kapufi amefika katika tukio hilo  na kulaani kitendo hicho huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa katika vyombo husika ili  vyombo hivyo viweze kushughulikia.

Aidha mh Kapufi amevitaka  vyombo vyote vinavyohusika na kutoa haki kwa jamii ikiwemo polisi na mahakama kutenda haki kwa wananchi ili kuondoa hasira kwa wananchi pindi wanapokuwa hawajatendewa haki.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


GWANGALALAA 2
Polisi na wananchi wakizima moto uliokuwa ukiendelea kuwaka ili kutambua mabaki ya miili.
GWANGALALAA 3
Nyumba ya Marehemu Franco Mganda ilivamiwa na watu wanaodaiwa kupinga uvuvi haramu na kuanza kubomoa kabala ya Polisi kufika.
GWANGALALAA 4
Mkazi mmoja ambaye alijeruhiwa wakati Polisi wakisambaza watu kutovamia nyumba ya Marehemu Franco.
GWANGALALAA 5
Tenga la samaki wanaodaiwa kuvuliwa kwa sumu alilobeba marehemu Franco.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina