Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-09-16

LIPULI FC YAITISHA AFRICAN SPORTS

Klabu ya Lipuli ya mkoani Iringa imetamba kuwa itahakikisha inaanza kwa ushindi dhidi ya African Sports ‘Wanakimanumanu’mchezo wa daraja la kwanza inayotarajia kuanza Septemba 24 mwaka huu ambako watawakalibisha vijana wa Tanga.

Akizungumza juu ya hatima hiyo,Mratibu wa Mazoezi na pia ni Msimamizi wa Usajili,Haruna Saleh,amesema kuwa wamejianda kuanza vizuri msimu huu katika Ligi hiyo kwani wamefanya maandalizi ya kutosha na kambi yao waliifanyia Dar es salaam katika uwanja wa Karume wakiwa chini ya Kocha Mkuu Richard Amache anayekinoa kikosi hicho.

“Kilichobaki ni kuwaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa kuja kuwapa hamasa ya ushindi wachezaji wao ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuipandisha Ligi Kuu msimu ujao kwani wanaamini ligi itakuwa ngumu kwa kila timu kutaka kupanda Ligi”alisema Saleh

Lipuli wataanza kampeni yao ya kutaka kupanda Ligi kwa kuwakaribisha Wana kimanumanu ambao msimu uliopita waliweza kushuka daraja kutokana kuwa na migogoro ya Uongozi na kupelekea timu tatu za Tanga kuweka rekodi Dunia kwa kushuka kwa pamoja ambazo zilikuwa ni African Sports,JKT Mgambo na Coastal Union.


Hata hivyo Uongozi wa timu hiyo wanajivunia kuwa na wachezaji vijana ambao watasaidiana na wakongwe na uwepo wa mchezaji mkongwe wa zamani wa Simba Salum Machaku,utawapa hamasa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo kwani ana uzoefu wa kutosha na soka la Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina