Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina

Search This Blog

Breaking

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

TANGAZA NASI HAPA


2016-09-10

Lulu aandika ujumbe mzito Instagram, kumtakia heri ya kuzaliwa Mpenzi wake 'Majay'

Baada ya Wadau mbalimbali pamoja na watu wa karibu wanamtakia Majay, heri ya mafanikio katika maisha yake,katika siku yake ya kuzaliwa. 
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na bosi huyo, amekuwa ni mmoja kati wa watu waliomtumia ujumbe wa heri ya mafanikio huku ujumbe wake ukionyesha ukaribu wa kimahusiano zaidi.
 
“Juhudi zako, uchapakazi na ukarimu ni vitu vichache tu kati ya vingi ninavyojivunia na nakujifunza kutoka kwako, I think sisi ni perfect Combo,” aliandika Lulu instagram.
 
Aliongeza, “Nikiwa mkubwa nataka kuwa kama wewe bosi wangu (I mean kuwa CEO na vitu kama hivyo) Juhudi zako tunaziona, tuko nyuma yako na tunakuombea mafanikio zaidi na zaidi. Yesu Wangu akutunze kwa ajili yangu na familia yetu kwa ujumla. Happy birthday baba G, My successful,”
 
Tetesi za mahusiano ya Majay na Lulu zilishika kasi zaidi baada ya wawili hao kuongozana kwenda Nigeria katika utoaji wa Tuzo ya Africa Magic Viewers Choice (MVCA) 2016.

No comments:

Post a Comment

Tunakupa habari motomoto na uchambuzi wa kina